TUFANYE KAZI KWA UBORA NA WAKATI-MHANDISI KAMWELWE (MB)


Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akitoa neno la utangulizi katika kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wa wizara na taasisi zake leo. Prof. Mkumbo amesisitiza utoaji wa huduma na utekelezaji wa miradi mbalimbali inayowalenga wananchi wa Tanzania ni picha inayojieleza kuwa serikali ipo na wananchi ndio namba moja katika huduma hizo. 
Sehemu ya watendaji waliohuduhuria kikao hicho wakimsikiliza Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isac Kamwelwe (Mb), hayupo pichani.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiongea na watendaji wa wizara na taasisi zake. Mhe. Jumaa amesisitiza kazi ifanyike kwa pamoja na kufikia lengo la kumtua mama ndoo ya maji nchini. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isac Kamwelwe (Mb) akisalimia na watendaji wa wizara na taasisi zake, kabla ya kuongea nao kuhusu utekelezaji na hatua zilizofikiwa katika kazi na miradi inayiohusu huduma ya maji  nchini. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isac Kamwelwe (Mb) akiongea na watendaji wa wizara, pamoja na taasisi zake (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika ofisini kwake Dodoma leo. Waziri Kamwelwe katika kikao hicho amesisitiza kufanya kazi kwa ubora, ndani ya muda mfupi  na kutoa huduma kwa wananchi ndio jambo la msingi

Comments

Popular posts from this blog

CONSULTANCY SERVICES FOR DEVELOPMENT AND IMPLEMENTATION OF LABORATORY INFORMATION MANAGEMENT SYSTEM (LIMS)

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI MHE. MHANDISI KAMWELWE (MB) ASIKILIZA KERO ZA MAJI CHAMWINO

WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI KUHAMIA KATIKA JENGO LAKE - PROF. MKUMBO